Maajabu 19 ya mbegu za maboga Kiafya Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi. Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 19 yafuatayo: 1. UGONJWA WA MOYO Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo. Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3. 2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili. Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili. 3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho. Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho. 4. KINGA YA KISUKARI Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia. Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari. Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa. 5. DAWA BORA YA USINGIZI Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’. Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini. Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi. Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu. 6. DAWA BORA YA UVIMBE Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation). Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye. Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu. Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini. 7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto. 8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’. Hii ni ripoti mhimu kuliko zote umewahi kusoma kuhusu Saratani ya tezi dume mpaka sasa. Nitakuonyesha ni kwanini madini haya yanachukuliwa kama ndiyo dawa bora zaidi katika kuzuia na kutibu Saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) ugonjwa ambao unaongoza kwa kuua wanaume duniani kwa sasa. Madini ya saliniamu ni dawa ya Saratani ya tezi dume ulikuwa huifahamu bado Kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kiasi cha madini ya Saliniamu (selenium) ulichonacho mwilini mwako na ugonjwa wa kansa. Labda unaweza kupima kwanza kuona kama una kiasi cha kutosha cha madini haya kwenye mwili wako na ikiwa yapo chini ya kiwango kuna uwezekano mkubwa kuwa ndiyo sababu ya wewe kuugua huo ugonjwa wa tezi dume. Dozi yake pia ni rahisi, unahitaji kutumia kiasi cha 200 micrograms cha madini haya kwa siku na utaweza kupunguza uwepo wa ugonjwa huu kwa zaidi ya asilimia 63. Asilimia 63 siyo jambo la kitoto si ndiyo? Sasa yanafanyaje kazi haya madini? Kwahiyo utakuwa unataka kuniuliza yanafanyajefanyaje sasa haya madini ili kuzuia na hata kutibu saratani ya tezi dume? Sikia. Madini haya yanayo uwezo wa kuzizuia seli za kansa kuzaliwa na kujizidisha mwanzoni kabisa mwa kuundwa kwake. Kwahiyo kansa inazuiliwa tangu mwanzoni inapotaka kutokea na madini haya ya saliniamu. Utakubaliana na mimi sasa kwamba hii ni ripoti mhimu zaidi kuhusu saratani ya tezi dume umewahi kuisoma kwamba madini ya saliniamu yanaweza kuizuia saratani ya tezi dume kutokea kwakuwa ugonjwa huu ndiyo ugonjwa unaoongoza kuua maelfu ya wanaume kwa sasa. Kabla hujaondoka, subiri kidogo. Siyo kwamba madini haya yanazuia tu seli za saratani ya tezi dume kutokea …. Bali pia ni dawa bora kabisa kwa kutibu ugonjwa huu. Endelea kusoma … Tafiti nyingi zimeendelea kuthibitisha kwamba madini ya saliniamu yanaweza kusaidia kupunguza kuongezeka kwa saratani na hata kuitibu kabisa ikiwemo saratani ya tezi dume kwa watu ambao tayari wanaugua ugonjwa huu. Na watafiti wamegundua kuwa nguvu ya madini ya saliniamu inakuwa kubwa zaidi ikitumika sambamba na vitamini C, vitamini E na beta carotene! Sasa hii saliniamu ubora wake inategemea na udongo ambako vyakula vyenye madini haya vinalimwa. Kwa mfano kwa sasa utaona maeneo mengi ya Ulaya na hata Amerika ardhi haina uwezo huo kama ile ya kwetu hapa Afrika na Tanzania. Kwahiyo sisi tuna uwezo mkubwa wa kupona saratani ya tezi dume kirahisi zaidi kuliko wenzetu wazungu. Wanaume wanaotumia kiasi kingi cha madini ya saliniamu, vitamini C na E wana uwezekano mdogo sana wa kuugua ugonjwa wa saratani ya tezi dume. Kwahiyo, mpaka sasa unapotaka kujitibu kansa ya tezi dume madini ya saliniamu yawe ni namba moja yako katika vitu unavyotumia kila siku. Utapata wapi sasa haya madini ya saliniamu? Namna rahisi ni kutumia dawa lishe maalumu (supplements) ambazo huandaliwa viwandani hasa kwa ajili ya watu wanaoishi katika nchi ambazo udongo wao hauna madini haya ya saliniamu kwa wingi. Kwa wewe mwenzangu ambaye Mungu bado amekujaalia kuwa bado na ardhi nzuri madini ya salianiamu yanapatikana, ukitumia vyakula vifuatavyo kila siku ni hakika utapona ugonjwa huu na ushuhuda utaniletea. Vyakula vyenye madini ya saliniamu kwa wingi ni pamoja na Mbegu za maboga. Sehemu kubwa ya Ulaya mbegu za maboga zinatumika kama dawa kamili ya kutibu saratani ya tezi dume. Mbegu hizi zina kiasi kingi cha madini ya saliniamu, madini ya zinki na madini mengine mhimu yaliyothibitika kudhibiti saratani ya tezi dume. Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume. Wanaume kazi ni kwenu. 9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado. Mbegu za maboga zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili. Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako. Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? (a) Unga wa Mbegu za maboga una kiasi kingi cha magnesium Moja ya madini ambayo ni mhimu sana ili kuwa na afya bora ya mbegu za mwanaume ni magnesium. Magnesium ni madini ambayo ni mhimu sana katika kdhibiti msongo wa mawazo na yana uwezo pia wa kudhibiti vizuri sana shinikizo la damu na kuwasaidia wanaume kupata usingizi mzuri. Kama tujuavyo kuepuka msongo wa mawazo (stress) ni njia moja nzuri sana ya kuwa na mbegu za kiume zenye afya na ubora wa hali ya juu. (b) Unga wa mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha omega-3 Ili kuzalisha mbegu zenye ubora wa hali ya juu wanaume wanahitaji mafuta mazuri yenye Omega 3 ambayo hupatikana pia kwa baadhi ya samaki hasa samaki ajulikanaye kama kibua (salmon). Lakini unafahamu pia kwamba unaweza kupata Omega 3 nzuri zaidi kwa kutumia unga wa mbegu za maboga?. Omega 3 siyo tu itakusaidia kuzalisha mbegu nzuri bali pia itakusaidia kuziweka sawa homoni zako na kuweka afya nzuri ya mwili wote kwa ujumla. (c) Unga wa Mbegu za maboga una Madini ya Zinki Kama tujuavyo madini ya zinki huongeza sana afya ya uzazi hasa kwa wanaume na tunaweza kuyapata madini haya mhimu kwa afya mbegu za mwanaume kwa kutumia tu unga wa mbegu za maboga kila siku. Kiasi cha kutosha cha madini ya zinki ni mhimu ndiyo kitu mhimu sana ili kuwa na mbegu za kiume zenye afya. Hakika afya ya uzazi ya mwanume itaimarika sana kama atakuwa akitumia vyakula vyenye madini haya. Kama wenza mnapanga kupata ujauzito ni mhimu sana kuwa na unga huu nyumbani na muutumie kila siku. (d) Unga wa mbegu za maboga unaondoa sumu mwilini Viondoa sumu mwilini ni mhimu sana ili kudhibiti vijidudu nyemelezi kuvamia mwili. Vijidudu nyemelezi (Free radicals) ni adui mkubwa kwa afya ya uzazi ya mwanaume ikihusisha pia afya ya mbegu zake. Kutumia vyakula safi vyenye uwezo wa kuondoa sumu mwilini ni njia madhubuti ya kuwa na mbegu bora kwa mwanaume. Hii ya kuondoa sumu inasaidia pia kuzalisha mbegu zenye ubora wa hali ya juu kabisa. (e) Unga wa mbegu za maboga unaimarisha afya ya tezi dume Afya ya tezidume na ubora wa mbegu ni vitu vinavyohusiana moja kwa moja. Kutumia unga wa mbegu za maboga kunasaidia mwanaume kuwa na afya nzuri ya tezidume zake na hivyo kuwa na mbegu nzuri mhimu kwa ajili ya uzazi. Lipo tatizo la kiafya kwa mwanume ambapo tezi dume zake moja au zote mbili zinaongezeka ukubwa tofauti na umbile lake la kawaida. Ukiacha na tafiti zinavyothibitisha kwamba unga wa mbegu za maboga unasaidia kuwapa wanaume tezidume zenye afya nzuri, matumizi ya unga wa mbegu za maboga unaweza kumsaidia pia mwanaume mwenye matatizo ya kiafya kwenye kibofu cha mkojo. (f) Unga wa mbegu za maboga unaongeza pia ujazo wa mbegu za mwanaume Matumizi ya mara kwa mara ya unga wa mbegu za maboga siyo kwamba yanasaidia tu kuboresha nguvu za kiume kwa wanaume bali pia husaidia kuongeza ujazo (sperm count) wa mbegu hizo na ubora wake. Kazi hii hasa huwezeshwa na unga wa mbegu za maboga kutokana na kuwa na kiasi cha kutosha cha protini, omega 3, zinki, magnesium, na vitamini E ndani yake. Hivyo ni wazi lazima utauhitaji unga huu kama wewe ni mwanaume unayejiandaa kupata mtoto. (g) Unga wa mbegu za maboga unasaida kuongeza kasi ya mbegu za kiume Mbegu bora za kiume zinahitajika pia ziwe na uwezo wa kusafiri na kukimbia kwa kasi inayohitajika ili kuvifikia via vya uzazi vya mwanamke na yai tayari kwa kurutubishwa. Bila mbegu kuwa na uwezo huu wa kukimbia ni ngumu kwa mbegu hizo kuogelea, kulifikia na kulirutubisha yai la mwanamke. Katika kesi kama hii unga wa mbegu za maboga na madini yake mhimu, protini na vitamini mbalimbali utakusaidia kuboresha spidi au kasi ya kukimbia ya mbegu zako (sperm motility). (h) Unga wa mbegu za maboga unaongeza ujazo wa mbegu Ukiacha ubora wa mbegu (quality), wingi wa mbegu (sperm count), na uwezo wake wa kukimbia (sperm motility), wanaume wanahitaji pia kiasi fulani cha mbegu (zisiwe chini ya milioni 20). Ndiyo kiasi hicho cha wingi wa mbegu ni mhimu na kinahitajika ili kuziwezesha mbegu hizo kuweza kubeba na kusafirisha kirahisi mbegu za uzazi za mwanaume kwenda kwenye via vya uzazi vya mwanamke na kulifikia yai kwa ajili ya utungishaji wa mimba. Viinilishe vilivyomo kwenye unga wa mbegu za maboga vinauwezesha mfumo wa uzazi wa mwanume kutengeneza mbegu za kutosha na zenye ubora unaohitajika ili kutungisha ujauzito. 10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya. Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako. Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance). Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’. Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa. 11. Huzuia mchanga kwenye kibofu cha mkojo Faida nyingine ya kushangaza kuhusu mbegu za maboga kiafya ni ule uwezo wake wa kuzuia mchanga au mawe kwenye kibofu cha mkojo. Kinachofanya hili liwezekane kupitia mbegu hizi ni kule kuwa na kiasi kingi cha ‘phosphorous’ ambayo ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo. Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili. 12. Huimarisha afya ya mifupa Kadri umri unavyoongezeka ndivyo na uwezo na uimara wa mifupa yako unavyopungua. Imefahamika sasa kuwa madini ya kalsiamu peke yake siyo kitu kinachoimarisha afya ya mifupa. Kuna madini na vitamini vyngine mhimu ili kuimarisha afya ya mifupa. Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na viinilishe vingine vingi mhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis). 13. Zinasaidia kuweka sawa shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu ni moja magonjwa sababishi ya vifo kwa watu wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo. Mbegu za maboga ni kitu mhimu kuongezwa katika mlo kwa watu wote wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu. Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili mhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini. 14. Zinaimarisha afya ya ubongo Kadri unavyoendelea kukua ndivyo na uwezo wa ubongo wako unavyopungua. Hata hivyo bado unayo nafasi ya kuzuia hilo kama utaishi na kula vizuri. Mbegu za maboga asidi mafuta ya Omega 3 zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘alpha-linolenic acid’ ambazo ni mhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo. Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo. 15. Zinaweka sawa Ph ya mwili Mwili unaweza kuwa katika hali mbili, ama katika asidi au katika alkaline (Ph). Mwili unapokuwa na asidi nyingi ndipo unapopatwa na magonjwa mengi kirahisi zaidi. Magonjwa hayo ni pamoja na maumivu ya mifupa, saratani, kisukari, vidonda vya tumbo, kichwa kuuma nk Hivyo ni mhimu chakula chako kiwe kwa sehemu kubwa ni chakula chenye alkalini na si asidi (tindikali) ili kukusaidia ubaki na Ph (Potential Hydrogen) ya 7.4 mara nyingi. Kumbuka chochote chini ya 7 Ph ni asidi. Mbegu za maboga ni moja ya vyakula vizuri zaidi vyenye alkalini ambavyo unatakiwa kuvijumuisha kwenye mlo wako. 16. Zinatibu tatizo la upungufu wa damu Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma. Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito. Hili linazifanya mbegu hizi kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaopata tatizo la upungufu wa damu unaotokana na kupungua kwa madini ya chuma mwilini. 17. Zinasaidia kupunguza uzito wa mwili Weka pembeni vyakula vyenye sukari nyingi na badala yake tafuna mbegu za maboga. Kinachotokea hapa ni kuwa mbegu hizi zinao uwezo wa kukuacha ukijisikia umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula vyakula vingine feki. Nyuzi nyuzi nyingi katika mbegu hizi zinazifanya kuwa chakula kizuri kuongezwa kwenye chakula chako cha asubuhi. Hata hivyo sababu zina protini nyingi iwapo utazidisha kula unaweza kuongezeka uzito na unene badala ya kupungua hivyo uwe makini. 18. Zinarahisisha uponyaji wa vidonda Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi. Kiais kingi cha vitamini A kwenye mbegu za maboga kinaweza kuwa msaada kuhamasisha uponyaji wa vidonda kwa mjibu utafiti mmoja uliofanywa na jarida moja la chuo cha afya ya ngozi nchini Marekani ‘Journal of the American Academy of Dermatology’. Kwa mjibu wa utafiti, vitamini A ndani ya mwili inaweza kuvutia mfumo wa mwili kujiripea wenyewe ndani kwa ndani bila kuhitaji dawa. Kama unasumbuliwa na vidonda au kidonda kwa muda mrefu hebu weka mazoea ya kutumia mbegu za maboga mara kwa mara na hutachelewa kuona uponyaji ukifanyika. Hii ni kweli ukizingatia pia mbegu hizi zinaongeza sana kinga ya mwili. 19. Zinasaidia kupevusha mayai ya uzazi kwa mwanamke Madini ya saliniamu yanahitajika kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa kromozoni katika mayai ya uzazi. Saliniamu ni madini ambayo hupatikana kwa wingi katika mbegu za maboga na kazi yake hasa ni kuondoa sumu na kuulinda mwili dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa na hivyo kuruhusu uzalishwaji mzuri wa mayai. Na watafiti wamegundua kuwa nguvu ya madini ya saliniamu inakuwa kubwa zaidi ikitumika sambamba na vitamini C, vitamini E na beta carotene! Faida nyingine ya mbegu za maboga katika afya ya mayai ni pamoja na kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya chuma. Madini ya chuma ni mhimu sana linapokuja suala la afya bora ya mayai ya uzazi. Kama mwili wako una upungufu wa madini ya chuma itakuwa vigumu wewe kupata ute wa uzazi. Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara. Namna nzuri ya kula mbegu za maboga: Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha. Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku. Unaweza pia kuzisaga na mashine maalumu au kuzitwanga katika kinu na utapata unga wake na utumie kijiko kikubwa kimoja kutwa mara 2 asubuhi na usiku kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji au kwenye mtindi au kwenye maziwa fresh au kwenye mchuzi wa mboga yoyote au unaweza pia kuchanganya kwenye wali na unaweza pia kutumia kama mafuta yako mbadala ya kupikia kwa vyakula vingi. Unaweza pia kuchanganya kwenye unga wa lishe wa mtoto